Na Mwandish wetu
MWANAMZIKI Mkongwe nchini Maalimu Ngurumo amefariki dunia leo Jijini Dar es Salaam.
Ngurumo amefariki wakati akiwa akipata matibabu ya ugonjwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akizungumza kwa njia ya simu Mpiga Gitaa na Kinanda wa bendi ya Msondo, Abuu Ridhwani (Toto) alisema taarifa za awali zinasema Mzee Ngurumo alipelekwa hospitali ya Muhimbili toka jana baada ya hali yake kuwa sio mzuri.
Taarifa zinasema kuwa msiba utakuwa Nyumbani kwake Tabata Geleji na mipango ya mazishi itafanya hadi pale familia itakapo kutana na mazishi ya kuwa nyumbani kwake Kisarawe katika kijiji cha Masaki.
Hadi tunaingia mtamboni timu nzima ya kusiniblog inaelekea Tabata na hivyo tutaelezana kila kitu kitakachoendelea
Inna Lillah Wainnah Illahi Raajiun .
|
No comments:
Post a Comment