Kwa habari zaidi kuhusu ORBIT tembelea tovuti ya: www.orbit-tz.com
KWA MAONI AU USHAURI TUTUMIE KWENYE E-mail: kusinileo@gmail.com

Thursday, 16 July 2015

TIMU ZA KAGAME ZAWASILI

Wachezaji wa timu ya Al Shandy ya Sudani wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  (JNIA) jijini Dar  es Salaam

Timu zote zinazoshiriki michuano ya Kombe la Kagame zimeaza kuwasili kwa ajili ya mashindano ya Kagame yanayotarajia kuanza  siku ya jumamosi.Akizungumza wakati mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa JNIA Kiongozi wa msafara wa timu ya Al Shandy ya Sudani alisema ana kuja kupambana ingawa safari hii wamekuja na vijana wadogo wa kikosi cha pili cha timu hiyo na alisema anahofia zaidi timu za Yanga na Azamu kwa kuwa zitakua zikipata sapot kutoka kwa Mashabiwao
Hatya hivyo bila shaka kufikia jioni vikosi vyote vya timu 13 vitakuwa vimefika nchini Tanzania. Timu zote zinatakiwa kujilipia gharama za usafiri huku mambo mengine yakifanywa na waandaaji.
Na kama ndiyo kwanza unasikia basi fahamu tu kuwa vilabu 13 kutoka ukanda wa Afrika masharik na kati vitakuwa vikichuana ili kuutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame ambalo linaenda sambamba na mgawanyo wa dola elfu 60 za kimarekani kutoka kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame. Tayari Timu ya wanamichezo wa Kusini Blog  imeanza kuifuatilia michuano hiyo na tutakuletea mambo yote.

No comments:

Post a Comment