Gesi asilia yainua mikoa ya kusini kimaendeleo
Na Kusini gesi
Mikoa ya kusini yaanza kunufaika na uwekezaji wa gesi Asilia Katika uwekezaji wa sekta hiyo
Moja ya Wilaya iliyopo katika mikoa ya kusini , Kilwa imeanza kunufaika kwa kukua kiuchumi kutokana na kile kinachozalishwa kuingia katika wilaya hiyo.
Akizungumzia maendeleo ya wilaya ya Kilwa, Mkurugenzi Mtendaji,Adoh Mapunda alisema kugundulika kwa gesi katika Wilaya Kilwa kumefanya kupiga hatua ya kiuchumi na kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo.
Alisema awali Halmashauri ya Kilwa ilikuwa inakosa mapato yatokanayo na gesi kutokana na visingizio mbalimbali tangu mwaka 2005 na kufanya halmashauri kuchukua jitihada mbalimbali ambazo zilifanyaka kudai haki hiyo ndipo mwaka 2012 Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kukubali deni lote tangu 2005 la sh.milioni 608.8.
Adoh alisema baada ya kulipwa fedha hizo kampuni ya Pan African Energy inayochimba Gesi hiyo katika Kijiji cha Songongo iliendelea kulipa ushuru wa tozo la huduma ya asilimia 0.3,
Aidha alisema tangu waanze kupokea fedha hizo kutoka kampuni ya Pan African Energy na kutoa fedha hizo asilimia 20 katika kijiji ambacho gesi inazalishwa ambapo wamepata jumla ya sh.milioni 139 ambazo zinaendeleza huduma mbalimbali za kijamii.
Mapunda alisema Wilaya hiyo imeanza kunufaika na uwekezaji kutokana na kile ambacho kinazalishwa kutolewa asilimia 2.
Alisema Kilwa ilikuwa nyuma kiuchumi katika miaka nyuma lakini kutokana na kupatikana kwa gesi umeweza kukua na kuongeza pato la wilaya pamoja na kuwa na mipango ya uongezaji huduma za jamii kwa jamii hiyo.
Mapunda alisema wilaya ilikuwa inategemea Kilimo cha mazao ya ufuta ,Mahindi,Mtama ,Mpunga pamoja na shughuli za uvuvi ambapo hayakuweza kuongeza mapato.
Alisema gesi imefungua uchumi ukurasa mpya ambapo baadhi za huduma za zimeboreshwa katika sekta ya maji ,Hospitali na miradi mingine inaendelea kubuniwa.
Alisema katika Maendeleo ya kutokana na gesi ya wilaya hiyo ni kujenga Hospitali kubwa ambayo itahudumia wananchi wa Kilwa pamoja na Wilaya jirani.
Mapunda alisema Kilwa ya sasa sio sawa na ya zamani kutokana na maendeleo yaliyopo pamoja na fursa zingine ambazo zimejitokeza kutokana na gesi hiyo kuanza kuchimbwa.
“Kazi iliyopo kwa watendaji wa Kilwa ni kusimamia mapato yanayotokana na gesi katika kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao,”alisema Mapunda.
Alisema katika miradi mingine imeibuka katokana na maendeleo ya gesi pamoja kupima viwanja ambapo viwanja hivyo wataviuza na thamani imeweza kuongezeka.
|
No comments:
Post a Comment