Kwa habari zaidi kuhusu ORBIT tembelea tovuti ya: www.orbit-tz.com
KWA MAONI AU USHAURI TUTUMIE KWENYE E-mail: kusinileo@gmail.com

Monday, 24 March 2014

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Dk. Aloyce Nzuki asimamishwa

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Dk. Aloyce Nzuki asimamishwa.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk.Aloyce Nzuki.
Kusimamishwa kazi kunatokana bodi ya wakurugenzi wa bodi ya utalii kutokuwa na imani ya utendaji wa mkurugenzi huyo.
Nyalandu alisema nafasi yake itangazwe mapema ili watu wenye sifa waombe kwa ajili ya kuingoza bodi hiyo.
Nafasi yake itakaimiwa na Devotha Mdachi mpaka atakapo tangazwa mkurugenzi mpya kuendeleza kutangaza utalii ndani na nje.

No comments:

Post a Comment