Timuya soka ya Simba leo imezidi kuwazoofisha mashabiki wao kwa kuchapwa bao 1-0 naCoastal Union kutoka Tanga katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam .
Wakicheza Uwanja wa Nyumbani Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, mbele ya mashabiki wao wamejikuta wakikubali kulala kwa Bao 1-0 kutoka Tanga, Coastal Union.
Bao la ushindi la Coastal Union lilifungwa katika Dakika ya 44 na Hamad Juma kwa Shuti kali
Matokeo haya yameipandisha Coastal na kukamata Nafasi ya 6 na kuiacha Simba ikigaagaa Nafasi ya 4 ikiwa Pointi 6 nyuma ya Timu ya Tatu Mbeya City, 7 nyuma ya Yanga na 11 nyuma ya Vinara Azam FC huku wakiwa wamebakiza Mechi 4 kumaliza Ligi.
Simba ambayo haina mwenendo mzuri toka ilipomtimuwa kocha wao King Kibadeni aliyethubutu kuwaamini vijana wadogo lakini timu hiyo kwa sasa ni kama bora liende tu wanasubiri ligi ifikie ulingoni na wajipange kwa vingine mwakani
Wakati huohuo timu ya Soka ya Azam FC Wana lamba lamba wamewachapa bao 1-0 timu ya wafunga Buti ya JKT Oljoro Katika Uwanja wa Azamu Complex Chamanzi na kuendelea kujiimarisha kileleni
Ushindi huu umeifanya Azam FC ipae kileleni ikiwa na Pointi 47 kwa Mechi 21 na kuiacha Yanga ikiwa Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 43 kwa Mechi 20.
No comments:
Post a Comment