Kwa habari zaidi kuhusu ORBIT tembelea tovuti ya: www.orbit-tz.com
KWA MAONI AU USHAURI TUTUMIE KWENYE E-mail: kusinileo@gmail.com

Monday 28 April 2014

MAONYESHO YA WIKI YA ELIMU (EDUCATION WEEK) KUFANYIKA DODOMA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                   JUMA LA ELIMU (EDUCATION WEEK)



Sekta ya Elimu ni mojawapo ya sekta sita zilizohusishwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN), Sekta nyingine ni Maji, Nishati, Fedha, Kilimo na Usafirishaji.

Sekta hizi zilishiriki katika kubaini changamoto na kuandaa mikakati ya kuondoa changamoto hizo. Kila sekta ilikaa kwa mtindo wa Maabara   (Lab) mwezi Februari 2013 kwa kushirikisha wataalam mbalimbali  kutoka serikalini, Wafadhili, vyuo vikuu, wastaafu na  Jumuia za Kiraia (CSO). Sekta ya Elimu ilikuwa na wataalam 34. Wataalam hao walijadili changamoto zinazokabili sekta hizo  na kupendekeza mkakati wanamna ya kuzitatua changamtoo hizo.

Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) uliandaa vigezo vya kuinua kiwango cha ubora wa elimu kwa kuweka malengo ya viwango vya ufaulu vitakavyofikiwa mwaka 2013 asilimia 60% mwaka 2014 asilimia 70 na 80% mwaka 2015.
Maabara ya Elimu iliibua mikakati tisa (9) yenye malengo ya kuinua ubora wa Elimu. Mikakati hiyo ni:-

1.    Upangaji wa shule kitaifa kwa kuzingatia matokeo
2.    Utaratibu wa kutoa tuzo kwa shule
3.    Kiongozi cha usimamizi wa shule
4.    Mtihani wa Taifa wa kupima Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesaba
5.    Mafunzo ya Walimu katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesaba
6.    Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji
7.    Ujenzi wa miundombinu muhimu ya shule
8.    Ruzuku ya uendeshaji shule
9.    Kuinua motisha kwa walimu

Utekelezaji wa mikakati hii upo katika hatua mbalimbali na inatekelezwa kwa ushirikiano kati ya OWM TAMISEMI na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi.

Maadhimisho ya Juma la Elimu ni Matokeo ya Utekelezaji wa Mkakati wa kutoa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri katika Mtihani wa  Taifa wa Darasa la Saba na Kidato cha Nne 2013 ili kutoa hamasa kwa jamii kushiriki katika kutoa Elimu bora

Mkoa wa Dodoma umepewa dhamana ya kuwa Mwenyeji wa Maadhimisho hayo Kitaifa ambapo Uzinduzi utafanywa tarehe 3/5/2014  na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Aidha Mgeni Rasmi siku ya kilele tarehe 10/05/2014 (National Award Day) anatarajiwa kuwa Mheshimiwa, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Halmashauri zote nchini zimeelekezwa kufanya Maadhimisho haya tarehe 3/5/2014 hadi 4/5/2014, Mikoa tarehe 7/5/2014 hadi 8/5/2014.

Ili kufanikisha maadhimisho haya, OWM – TAMISEMI  imewajibika kwa shughuli zifuatazo.

1.     Kukusanya taarifa za hatua ya maandalizi  kila Alhamisi ya kila wiki Kimkoa, kuanzia kupitia mtandao wa  TAMISEMI (pmo-ralg.go.tz).

2.    Kuunda Kamati za maandalizi ya maadhimisho  ya Juma la Elimu kwa kuzijumuisha Halmashauri tatu (03) za Mkoa wa Dodoma ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Chamwino na Dodoma Manispaa na kuzisimamia katika utekelezaji wa maadhimisho hayo.

3.     Kushirikiana na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Wakurugenzi wa Halmashauri tatu za Dodoma kuandaa eneo la uzinduzi na kilele kwa ajili ya maadhimisho hayo.

4.    Kuwapa miongozo Mikoa na Halmashauri juu ya maadhimisho ya Juma la Elimu.

5.    Kuandaa gharama za nauli, malazi na chakula kwa ajili ya Wakuu wa Shule na wanafunzi wa Shule zilizofanya vizuri Kitaifa ambao wataalikwa kuja Dodoma kupokea Tuzo.
           

Kwa upande wa Mikoa na Halmashauri wanawajibika kwa yafuatayo;

1.     Kuwashirikisha wadau wote wa Elimu wakiwemo walimu, wazazi, wanafunzi, mashirika, TOMONGOSCO, CWT, TAHOSA, Vyombo vya habari na watu binafsi.

2.    Kuwashirikisha wanafunzi kuandaa maonyesho na michezo mbalimbali kama vile maigizo, ngoma, mashairi, ngonjera na vipaji maalumu.

3.    Kusimamia utoaji wa tuzo katika shule kwa walimu na wanafunzi.

4.    Kufanya uhamasishaji kwa kuandaa vipindi maalumu vya radio/TV ili kuhamasisha ushiriki wa wananchi wengi zaidi siku ya Tuzo ngazi ya Halmashauri na Mikoa.

Ofisi yanyu ina waagiza Makatibu Tawala wa Mikoa  kujitokeza na kuwapatia wananchi taarifa kupitia vyombo vya Habari juu ya uwepo wa juma la Elimu ngazi ya Mkoa na Halmashauri pamoja na kueleza shughuli zitakazofanyika. 

Mwisho niwaombe wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye juma la Elimu ngazi ya Halmashauri, Mkoa na Taifa.

Wakazi wa Mkoa wa Dodoma mnayo fursa kubwa na bahati ya kuwa na uzinduzi na kilele cha juma la Elimu kufanyika Dodoma hinyo mnaombwa kuhudhuria kwa wingi ili mjionee maadhimisho ya kwanza ya Juma la Elimu.


Imtolewa na Mhe. Majaliwa K Majaliwa (Mb), Naibu Waziri Elimu
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

April ,2014



No comments:

Post a Comment