Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo afungua kongamano la mafuta na gesi nchini jerumani
1-Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo akifungua kongamano hilo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha mada
juu ya fursa za uwekezaji nchini Tanzania katika sekta za mafuta, gesi ikiwa ni
pamoja na madini.
Mtaalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli
Nchini (TPDC) Bi Venosa Ngowi (kulia) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo (mwenye suti nyeusi) shughuli zinazofanywa na shirika
hilo kwenye maonesho yanayoendelea huko Berlin, Ujerumani. Pembeni ya Waziri ni
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo
Mtaalamu kutoka Wakala wa Jiolojia Nchini (GST)
Bi. Augustina Rutaihwa akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo (katikati) juu ya shughuli zinazofanywa na wakala huo. Kushoto
mwa Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe.
Philip Marmo akifungua kongamano hilo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo (Mb.) (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wajumbe anayewakilisha
wafanyabiashara kabla ya kufungua kongamano la mafuta na gesi linaloendelea
huko Ujerumani kama moja ya maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
No comments:
Post a Comment