Kwa habari zaidi kuhusu ORBIT tembelea tovuti ya: www.orbit-tz.com
KWA MAONI AU USHAURI TUTUMIE KWENYE E-mail: kusinileo@gmail.com

Wednesday, 7 May 2014

IPTL NA PAP YAISHANGAA Mtanzania KUDHALILISHA KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI

Mshauri wa sheria wa kampuni ya PAP na IPTL, Joseph Makandege akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kukanusha taarifa iliyotolewa na moja ya gazeti la kila siku kuwa kampuni hiyo iliihonga kamati ya Bunge ya Nishati na Madini
Na kusiniblog
Kamati za Uongozi wa kampuni ya  Pan Africa Power (PAP) ambao ni wamiliki wa kampuni ya kufua umeme ya  Independent Power Tanzania ltd (IPTL) wameshangazwa na taarifa zilizochapisha na gazeti la Mtanzania la Toleo namba 7451 la jumatatu ya 05-05 2014 yenye kichwa cha habari kinachosema “KASHFA MZITO KAMATI ZA BUNGE” akizungumza na blog hii Mshauri na mwanasheria wa kampuni hiyo ya IPTL ,Joseph Makandege alisema wao kama kampuni wamechukulia taarifa iliyochapishwa na gazeti hilo kama Uchochezi na udhalilishaji mkubwa kwa kamati za bunge  ya Nishat na Madini
Akifafanua zaidi Mkandege alisema Kamati hiyo ya bunge  walikutanao  katika ofisi ndogo za bunge mara mbili na baadae kamati hiyo walipanga kutembelea Mitambo iliyopo Tegeta na siku ya waliotembelea mitambo hiyo kamati iliwastukiza wakati uongozi wa juu wa kampuni hiyo ulikua safarini lakini walipokelewa na plant meneja ambaye aliwatembeza wabunge hao na taarifa kuwasilishwa kwa viongozi baada ya kurejea sasa huyo mtu aliyewapokwea  hana mamlaka yoyote kifedha kuweza kuipatia kamati hiyo   alihoji Mkandege.
Akiongeza alidai wao kama kampuni wanachukulia kama changamoto tuu na mbinu chafu za wapinzani wao kibiashara akitolea mfano kwa sasa wao wana uza Unit moja shilling 26-30 tofauti na wapinzani wao kibiashara.
Alisema wao wana mpango wa kupunguza bei ya umeme mpaka kufikia senti 6-7 kwa unity endapo serikali itawauzia gesi kwa centy 3 kama walivyoahidi.
Alielezea sababu za wao kuuza unity kwa bei ya chini hivi sasa kuliko wapinzani wao kuwa ni kwasababu wanatumia malighafi ya mafuta mazito Have Fuel Oil na wapo kwenye mchakato wa kubadilisha mashine ili kutoa nafuu zaidi kwa wananchi.
 

No comments:

Post a Comment