Kwa habari zaidi kuhusu ORBIT tembelea tovuti ya: www.orbit-tz.com
KWA MAONI AU USHAURI TUTUMIE KWENYE E-mail: kusinileo@gmail.com

Friday, 2 May 2014

MAKAMU WA RAIS DR.MOHAMED GHALIB BILALI AWASHA MWENGE MKOANI KAGERA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete. Picha na OMR



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kuuwasha rasmi wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo


Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian Masawe, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kukabidhiwa .


Vijana wenye dhamana ya kukimbiza mwenge wa Uhuru 2014, wakianza rasmi mbio hizo baada ya kuwashwa


No comments:

Post a Comment