|
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Usafirishaji wa
Mizigo Usangu Logistic,Ibrahim Ismaili ameitaka serikali kuwapima Madereva wa
magari kabla ya kutoa Leseni ili
kuepusha ajali zisizo na lazima na kuliepusha taifa hasara na wimbi kubwa la
walemavu wa viungo.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa
habari ofisini kwake jijini Dar es
Salaam .
Akifafanua zaidi Ibrahimu alisema ajali nyingi
nchini zimekuwa zikitokea kwa kusababishwa na uzembe wa madereva kwani mamlaka husika hutoa leseni lakini
hakuna mpango wa kutambua au kumpima muhusika kabla ya kupata leseni
Aidha alisema taifa linaingia hasara kila siku
kutokana nan ajali ambazo zingweza kuzuilika kutokana na madereva wengi kutokua
na elimu na kutumia kilevi wawapo kazini hali inayohatarisha usalama wao na
gari.
Pia aliwataka
Madereva kujenga tabia ya kusoma katika vyuo vinavyotambuliwa na mamlaka husika
pia kujali na kuzifata sheria za usalama barabarani kikamilifu
Vile vile alishauri serikali kupunguza Road block (vizuizi)
za barabarani kwani wakati wa kusafirisha mizigo kumekuwa na ucheleweshwaji wa
barabarani hali inayowapa usumbufu madereva wawapo njiani.
.
|
No comments:
Post a Comment