Kwa habari zaidi kuhusu ORBIT tembelea tovuti ya: www.orbit-tz.com
KWA MAONI AU USHAURI TUTUMIE KWENYE E-mail: kusinileo@gmail.com

Wednesday, 16 April 2014

BMTL YABADILI JINA LA KIBIASHARA KUWA COP CAT

 Bw Holtham akibadilishana Mawazo na wateja katika hafla hiyo
 
  Bw Holtham akiongea na wandishi wa habari
Baadhi ya wadau wakibadilishana Mawazo

BMTL yabadili jina la kibiashara na kuwa Copy Cat
.
KAMPUNI ya Business Machines Tanzania Limited (BMTL) imebadilisha rasmi jina lake la biashara kwenda kwenye kampuni yake mama ya Copy Cat katika harakati zake za kupanua wigo wa biashara nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa uzinduzi rasmi wa jina la biashara la Copy Cat nchini, Afisa Mtendaji Mkuu Mpya wa Kampuni hiyo, Bw Mike Holtham amesema kampuni inayofuraha ya kujiunga rasmi katika jina la kampuni mama ya makampuni hayo ya Copy Cat Afrika Mashariki.
“kampuni ya BMTL ilikuwa ni miongoni mwa kampuni ya Copy Cat kwa hiyo viongozi wamekutana wa Afrika Mashariki wameona ni fursa ya kipekee kuunganisha au kutumia jina moja la kibiashara (Brand) katika kujiimarisha katika biashara za kompyuta na ufundi na utengenezaji wa mifumo ya mitandao na mawasiliano nchini,” amesema Bw, Holtham
Amesema kuwa kubadilisha jina la kibiashara na jambo la kawaida katika mkakati wa kujiimarisha kibishara na kimasoko katika juhudi za kutafuta wateja wapya na kupanua wigo wa biashara ili kukuza mauzo ya ndani na nje ya nchi.
Bw, Holtham aliongeza kuwa kwa zaidi ya miaka 2o kampuni ya BMTL ilikuwa chini ya kampuni ya Copy Cat na imewakilisha vizuri katika soko la Tanzania kwenye maswala ya teknolojia na kompyuta.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mauzo, BMTL, Copy Cat, Avais Ansari amesema kuwa kwa zaidi ya miaka 50 kampuni hiyo imejikita kwenye maswala ya ulinzi wa kutumia teknolojia na uchapaji wa vitu mbalimbali kwa kutumia kompyuta hapa nchini.
“kubadilisha jina na kwenda kwenye kampuni mama ya Copy Cat ni mkakati tu kwa kibiashara katika jitihada ya kukuza na kupanua biashara zetu hapa Tanzania,” amesema Bw, Ansari
Amesema kampuni hiyo ipo pia katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia na Tanzania na wana mkakati wa kwenda nchi zingine kusini mwa jangwa la sahara.

No comments:

Post a Comment