Kwa habari zaidi kuhusu ORBIT tembelea tovuti ya: www.orbit-tz.com
KWA MAONI AU USHAURI TUTUMIE KWENYE E-mail: kusinileo@gmail.com

Wednesday, 16 April 2014

MZEE GURUMO AZIKWA

Rais Kikwete akiwafariji wafiwa
Rais Kikwete akimfariji Mtoto wa Marehemu.

Waumini wa Kiislamu wakimzika Maalim Gurumo .
Na Mwandish Wetu

MKONGWE wa muziki wa dansi nchini, Muhidin Mohamed Mwalimu Gurumo ‘Maalim Gurumo’ amezikwa jana kwenye makaburi ya kijijini kwake, Masaki, Kisarawe  Pwani.

 Gurumo aliyezaliwa miaka 74 iliyopita katika kijiji cha Masaki Kisarawe jana ndio ilikua siku yake ya Mwisho ambapo alizikwa kijijini kwao Masaki hapo hapo alipozaliwa

Gurumo ambaye alipitia bendi mbali mbali nchini ikiwemo ya Nuta ambae baadae ilijulikana Juwata,OTTU na sasa hivi Msondo Music Band pia Gurumo ni muasisi wa Bendi ya DDC mliman park Ngurumo na wenzake waliondoka juwata mwanzoni mwa miaka ya 80 na kwenda kuanzisha bendi DDC.

 Hata hivyo baadaye tena Gurumo alitoka DDC na kujiunga na OSS wana Ndekule.

  Maalim Gurumo ametunga na kuimba nyimbo nyingi akishirikiana na waimbaji mbali mbali wakiwemo Sulemani Mbwebwe,Athumani Momba ,Tx Moshi Wiliam ,

Wengine ni Jose Maina  ambao wote ni Marehemu pia aliimba na Shabani Dede ,Bichuka,Husseni Jumbe ,Eddo Sanga na wengine wengi ambao huwezi kumaliza kuwataja.

Miongoni mwa vijana waliobaatika kuimba na Gurumo ni kiongozi wa Bendi ya Exra Bongo,Alli Choki pale walipofanya remix ya nyimbo  za Gurumo.

Mwaka jana Gurumo alitangaza kustaafu muziki na kuahidi kutoa ushirikiano kwa vijana watakaotaka kumtumia kwa ushauri lakini tukio la kufurahisha ni pale msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond  alipomzawadia gari mzee huyo ambae katika maisha yake ya muziki hakuwahi kumiliki.

Akitoa neno la shukrani , Gurumo alisema”Katika maisha yangu sikuwahi kumiliki gari”. Wimbo ufuatao Gurumo aliongoza kuimba.

Wanangu woote Njooni kaeni chini ni wambie Maisha ya Sasa ni magumu tofauti na ya zamani
  Wakati wa ujana wangu mimi baba yenu Shati dukani shilingi sita unapata lakini sasa shilingi sita hata mkate hupati.

Kiitikio
Kwahiyo wanangu kuishi kutokana na wakati
Kwahiyo wanangu kuishi kutokana na wakati 

No comments:

Post a Comment