Kwa habari zaidi kuhusu ORBIT tembelea tovuti ya: www.orbit-tz.com
KWA MAONI AU USHAURI TUTUMIE KWENYE E-mail: kusinileo@gmail.com

Sunday, 30 March 2014

AJALI YAUA WATU 20 IKWIRIRI


Askari wa usalama Barabarani akiangalia mabaki ya Basi

Ajali mbaya imetokea katika kijiji cha  Mpapuka Akizungumza na Kusini gesi ,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,Ulrich Matei ,alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 2 :20  usiku katika eneo Mpapuka,Kibiti ,Wilayani Rufiji Mkoani Pwani
Alisema chanzo cha ajali hiyo kilitokana na gari yenye namba za usajili T 948 CUX  aina ya Hiace ambalo lilikuwa linapita Lori i lenye namba za usajili T 132 AFJ aina ya Tata ambalo lilikuwa limesimama  na kwenda kugongana uso kwa uso na gari  yenye namba za usajili T 774 CJW aina ya Center na kusababisha vifo vya watu 20.
Matei alisema waliofariki katika ajali hiyo wanawake wawili na wanaume 18 na majeruhi 10.
Kamanda aliwataja waliofariki katika ajali hiyo ni Situs ally Mtanga (32) Mkazi wa Ikwiriri,Nassoro Kajani (20)Mkazi wa Ikwiriri,
 Juma Kitambulio (30)Mkazi wa Mbagala,SalumuMakonde(50)Mkazi wa Charambe,ShabanBakari (30) Kondakta wa Hiace Mkazi wa Kibiti,Ustadh Kalilambwe 34 Mkazi wa Mbagala , Shafil Kipi ( 30) Mkazi wa Mbagala,Masud Abilal (27) Mkazi Mkuranga,Amin Mpemba (30) mkazi wa jaribu , japhet  jafet ponsian (24) mkazi wa Dar es Salaam,said aly china (21) mkazi wa kimanzichana.  wasabi sabil( 45) makazi wa mbagala .13 madadi hasan mangasongo (45) mkazi wa jarib, Ramadhan s. AlLy (23) mkazi wa Mbagala
Alisema wengine ni Abdalahaman yusuphu kihemke 45yrs mkazi wa kongowe fikiri said sauze  mkazi wa vikindu  seleman mcharazi (47) Mkazi wa mbagala.  mstafa s/? mkazi wa Mbagala , nywari mshigani mkazi wa Dar es Salaam , Hasan wasabi (18) mkazi kibiti na mmoja wa kike hajatambuliwa.


Aliwataja majeruhi ni Frenk sixmund (31)dereva  wa maliasili kibiti kaumia kichwani,Mohammed saleh ( 49) mkazi wa kibiti ,charlrs logasian maia (23) makazi wa kibiti,
Wengine Mohammed miaka (42) mkazi wa Dar esa salaam,Mniko magige (54) mkazi wa mkuranga,Khalid salum  (32)  mkazi wa Dar es salaam,Ahmad Yusuph miak (23) makazi wa kigamboni,Shomari Yusuph miaka 42) mkazi wa mburahati,Abdalaah Issa (25) mkazi wa mkuranga.

TIGO YA ZAMINI GULIO LA COCO BEACH KARIAKOO


 
GETHEM MIN SUPER MARKET NAO WALIKUWEPO
J

 
Shantalle Herbs Oil pia tulikua nao wauzaji wa vipodozi na Sabuni za Ukwaju kwa ajili ya Ngozi 

SHIVJI AONGOZA KONGAMANO LA WANA VYUO KUHUSU WAJIBU WA VIJANA KUENDELEZA MUUNGANO


PRF Issa Shivj akiongea katika kongamano hilo



Badhi ya wana chuo wakifatilia kwa makini kongamano la Kujadili jinsi kijana anavyoshirikishwa katika Mchakato wa Katiba mpya na  miaka 50 ya muungano.Picha na Kusinigesi



Saturday, 29 March 2014

Wakazi wa Kunduchi wamzika mama Mary Mtaita

Mama Mary Enzi za Uhai wake
Jeneza likiwa tayari kwa kuagwa


Watoto wakiwa na picha pamoja na mashada

Umoja wa wanakikundi cha KIWAMA wakiwa wamebeba jeneza la aliyekuwa mwanachama mwenzao

 
 
 
Washika dau nao walikuwepo kumpa tafu mwenzao


 
 
 
 
Wajukuu wakishiriki zoezi la mwisho la kuweka mashada ya maua.
 
Wakazi wa kunduch jijini Dar es walifurika kwa wingi nyumbani kwa Mama yetu mpendwa ,Mama Mary Mtaita katika ibada ya mwisho ya Mazishi iliyofanyika jioni hii
Akisoma historia fupi ya Marehemu Msemaji wa familia alisema maerhemu alizaliwa 1948 mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Same na kufariki siku ya tarehe 24-march 2014 kwa shinikizo la damu na leo siku ya tarehe 29 ndio siku tumempumzisha kwenye makazi yake ya milele.Marehemu ameacha watoto 7 na wajukuu 12
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa.
Ameen  
 
 
 


 


Friday, 28 March 2014

TMF YATOA VYETI KWA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UHANDISHI WA HABARI ZA KIUCHUNGUZI SEKTA YA GESI NA MADINI

Mfuko wa Vyombo vya Habari nchini (TMF).leo umetoa vyeti kwa wahandishi wa habari Wandamizi wa Habari za Uchunguzi katika sekta ya Madini na Gesi baada ya kupitia mafunzo ya miezi 3 yalioandaliwa na mfuko huo nchini Baadhi ya wahitimu walioshiriki Mafunzo hayo ni, Jastoni Binara ,Saidi Mmanga (Changamoto)Nambambael Mduma(Habari Leo),Felix Mwakyembe (Raia Mwema),Esther Meling,Sidi Mgumia,Deo Mush,John Bwire(Raia Mwema) na Shemax Ngurumela(The African) Aidha akizungumza wakati wa utoaji tuzo huo Mkurugenzi wa TMF ,Ernest Sungura alishauri Wahariri kuwatumia Wahandishi waliopitia mafunzo hayo Kwani wanauelewa mkubwa walioupata na kuacha tabia ya kukalia stori wanazoletewa na waandishi hao.

Thursday, 27 March 2014


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya mwaka 2012/2013 na mwaka 2013/2014, Waziri wa Nishati na Madini alitoa wito kwa wamiliki wa leseni za madini kuwataka kuzingatia sheria na kanuni zilizopo. Aidha, Waziri alitamka bayana kuwa wale wote watakaobainika kukiuka sheria  na masharti ya leseni zao wangefutiwa leseni.

Katika kutekeleza agizo hilo, wamiliki wa leseni 888 walipewa notisi za makosa katika kipindi cha mwaka 2012/2013; ambapo jumla ya leseni 160 za utafutaji na leseni moja ya uchimbaji wa kati zilifutwa. Aidha, leseni 268 za uchimbaji mdogo zilifutwa.  Kwa kipindi cha mwaka 2013/2014, wamiliki wa leseni 289 walipewa notisi za makosa. Kati ya leseni hizo, 211 zilikuwa za utafutaji mkubwa wa madini, leseni 78 zilikuwa za uchimbaji wa kati na leseni moja ya uchimbaji mkubwa wa madini ya makaa ya mawe katika eneo la Kabulo. Kutokana na taarifa hizo za makosa, jumla ya leseni 174 za utafutaji madini na leseni moja ya uchimbaji mkubwa zimefutwa kwa mujibu wa sheria.

Wizara hivi sasa imeunda Timu Maalum ya ukaguzi ambayo inatembelea maeneo yote ya utafutaji na uchimbaji wa madini, pamoja na maduka ya wafanyabiashara wa madini nchini ili kujiridhisha kama wahusika wanatimiza masharti ya leseni walizopewa. Timu hiyo imeanza kazi yake kwenye mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara na itaendelea na kazi hiyo katika maeneo yote nchini. Wale wote watakaobainika kukiuka masharti ya leseni, watapewa hati za makosa na leseni zao kufutwa iwapo watashindwa kurekebisha kasoro hizo.

Pamoja na hatua hizo, Wizara pia imeanza kudhibiti umilikaji wa maeneo makubwa ya leseni kwa kutowapa maeneo mapya wale ambao maeneo wanayoyamiliki hivi sasa yanazidi kilomita za mraba 2,000. Pia, Wizara  inaendelea kufuta leseni ambazo maeneo yake hayafanyiwi kazi na wamiliki wake.  

Tanzania imejaliwa hazina kubwa ya madini ya aina mbalimbali ambayo imevutia watu na kampuni nyingi kuomba leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini nchini. Umilikaji wa leseni za madini hapa nchini unaongozwa na Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na kanuni zake.

Kutokana na mvuto wa uwekezaji uliopo katika sekta ya madini, hadi sasa kuna jumla ya leseni 3,950 za utafutaji mkubwa wa madini, pamoja na maombi 3,677 ya leseni hizo. Aidha, kuna leseni 393 za uchimbaji madini wa kati na maombi 99 ya leseni za uchimbaji. Leseni za uchimbaji mdogo hadi sasa zinafikia jumla ya 35,717 na maombi 16,263.

Pamoja na uwingi huo wa leseni za madini, imebainika kuwa baadhi ya wamiliki wa leseni wanakiuka sheria ya madini kwa kuhodhi maeneo makubwa ya leseni, kukwepa kulipa ada, mrabaha na kodi kwa wakati na ama kushikilia maeneo yaliyo chini ya leseni zao bila kuyafanyia kazi. Hali hii inachelewesha ukuaji wa sekta, na kuikosesha Serikali mapato. Ni azma ya Wizara kuhakikisha kwamba speculators wote wanaachia maeneo wanayoyashikilia hivi sasa ili wawekezaji walio tayari kuyaendeleza wamilikishwe.

Tunapenda kuwaomba wamiliki wa leseni za madini kuzingatia wajibu wa kuyaendeleza maeneo ya leseni walizomilikishwa na Wizara ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.


Mhandisi Paul M. Masanja
KAMISHNA WA MADINI


UTANDAZAJI BOMBA LA GESI KUMALIZIKA JULAY


Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha michoro ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea eneo la ujenzi huo, Madimba, mkoani Mtwara. Wanaotazama ni wakaguzi hao, kutoka kushoto ni Prof. Longinus Rutasitara, Bibi Salome Kingdom, Bibi Florence Mwanri na Bw. Jordan Matonya.

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais ikijionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara


Vingozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Kulia) wakiangalia moja ya bomba la kusafirishia gesi. Bomba moja lina uzito wa tani tano na urefu wa mita 11.

 Na Saidi Mkabakuli 
Maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu kufuatia kuendelea vyema kasi ya kundaza bomba hilo. 
Wakizungumza na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Wahandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela na Mhandisi Omary Kitiku wamesema kuwa kasi ya sasa ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo kijiji cha Madimba, mkoani Mtwara inatia moyo na hivyo kuashiria kukamilika kwa mchakato huo kwa wakati. 
“Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 za bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam zimeshatandazwa hali inayokwenda sambamba na mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiki,” alisema Mhandisi Yagela. Kwa mujibu wa Mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiko hadi kufikia mwisho wa Julai kiwanda kinatakiwa kukamilika, na mpaka sasa, makazi ya wafanyakazi imekamilika. 

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mmoja wa viongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alisema kwamba kukamilika kwa bomba hilo kunatoa mwanya wa kukamilika kwa wakati uzalishaji wa umeme katika vituo vya Kinyerezi, jijini Dar es Salaam. 
“Kukamilika kwa bomba hili kunatoa fursa ya kwa Mradi wa kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 150 na Megawati 240 kwa kutumia gesi asilia vilivyopo Kinyerezi, jijini Dar es Salaam,” alisema Bibi Mwanri. 
Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16), Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati ambapo nguvu kubwa imewekwa katika uwekezaji wa miundombinu ya nishati ambapo utekelezaji wa ujenzi wa bomba la gesi Mtwara hadi Dar es Salaam unafanywa sambamba na ujenzi wa mitambo miwili ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi Dar es Salaam. Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. 
Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi.  Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa. Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.


MAFURIKO DAR

Magari yakipita katika maji yaliojaa barabarani katika Barabara ya Mwaikibaki jijini Dar es Salaam

Mkazi wa jiji akikatiza katika maji eneo la Hospitali ya TMJ


Wakisubiri maji yakauke waendelee na safari


Wizara ya Nishati na Madini yatoa Ufafanuzi juu ya Wavamizi wa Mgodi wa RESOLUTE T LTD wa NZEGA



Kamishina wa Madini wa Wizara ya Nishati na Madini, Eng Paul Masanja Akitoa ufafanuzi kwa wandishi wa habari kuhusu Wavamizi wa Mgodi wa kampuni ya RESOLUTE (T) LTD  wa Nzega katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Msemaji wa Wizara hiyo Badra Masuod
 


Kamishina wa Madini wa Wizara ya Nishati na Madini, Eng Paul Masanja Akitoa ufafanuzi kuhusu  Wavamizi wa Mgodi wa kampuni ya RESOLUTE (T) LTD  wa Nzega kwa wandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Msemaji wa Wizara hiyo Badra Masuod na kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini Eng John Nayopa
 

Wednesday, 26 March 2014

YANGA YAWAGALAGAZA WAJELA JELA

Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli

Emanueli Okwi akiwatoka walinzi wa Prisoni



Mashabiki wa Yanga wakishangilia goli



Mdau Mkuu wa Blog hii Kiongozi, Anthon Nyeupe  mwenye t shert ya bluu kulia akifatilia gemu

Gesi asilia yainua mikoa ya kusini kimaendeleo


Gesi asilia yainua mikoa ya kusini kimaendeleo
Na Kusini gesi
Mikoa ya kusini yaanza kunufaika na uwekezaji wa gesi Asilia Katika uwekezaji wa  sekta hiyo
 Moja ya Wilaya iliyopo katika mikoa ya kusini , Kilwa imeanza kunufaika kwa kukua kiuchumi kutokana na kile kinachozalishwa kuingia katika wilaya hiyo.
Akizungumzia maendeleo  ya wilaya ya Kilwa, Mkurugenzi Mtendaji,Adoh Mapunda alisema kugundulika kwa gesi katika Wilaya Kilwa kumefanya kupiga hatua ya kiuchumi na kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo.
Alisema awali Halmashauri ya Kilwa ilikuwa inakosa mapato yatokanayo na gesi kutokana na visingizio mbalimbali tangu mwaka 2005 na kufanya halmashauri kuchukua jitihada mbalimbali ambazo zilifanyaka kudai haki hiyo ndipo mwaka 2012 Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kukubali deni lote tangu 2005 la sh.milioni 608.8.
Adoh alisema baada ya kulipwa fedha hizo  kampuni ya Pan African Energy inayochimba Gesi  hiyo katika Kijiji cha Songongo iliendelea kulipa ushuru wa tozo la huduma ya asilimia 0.3,
Aidha alisema tangu waanze kupokea fedha hizo kutoka kampuni ya Pan African Energy na kutoa fedha hizo asilimia 20 katika kijiji ambacho gesi inazalishwa ambapo wamepata jumla ya sh.milioni 139 ambazo zinaendeleza huduma mbalimbali za kijamii.
Mapunda alisema Wilaya hiyo  imeanza kunufaika na uwekezaji kutokana na kile ambacho kinazalishwa kutolewa asilimia 2.
Alisema Kilwa ilikuwa nyuma kiuchumi katika miaka nyuma lakini kutokana na kupatikana kwa gesi umeweza kukua na kuongeza pato la wilaya pamoja na kuwa na mipango ya uongezaji huduma za jamii kwa jamii hiyo.
Mapunda alisema wilaya  ilikuwa inategemea Kilimo cha mazao ya ufuta ,Mahindi,Mtama ,Mpunga pamoja na shughuli za uvuvi ambapo hayakuweza kuongeza mapato.
Alisema gesi imefungua uchumi ukurasa mpya ambapo baadhi za huduma za zimeboreshwa katika sekta ya maji ,Hospitali na miradi mingine inaendelea kubuniwa.
Alisema katika Maendeleo ya kutokana na gesi ya wilaya hiyo ni kujenga Hospitali kubwa ambayo itahudumia wananchi wa Kilwa pamoja na Wilaya jirani.
Mapunda alisema Kilwa ya sasa sio sawa na ya zamani kutokana na maendeleo yaliyopo pamoja na fursa zingine ambazo zimejitokeza kutokana na gesi hiyo kuanza kuchimbwa.
“Kazi iliyopo kwa watendaji wa Kilwa ni kusimamia mapato yanayotokana na gesi katika kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao,”alisema Mapunda.
Alisema katika miradi mingine imeibuka katokana na maendeleo ya gesi pamoja kupima viwanja ambapo viwanja hivyo wataviuza na thamani imeweza kuongezeka.



Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue aongoza makatibu wakuu kutembelea Ujenzi wa Miundombinu ya Umeme Kinyerezi


Wakipata Maelekezo

Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jacobsen Elektro, Shaun Moore (kushoto) akiwaelezea jambo  makatibu wakuu wa Wizara waliongozana na Katimu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, waliotembelea kukagua ujenzi wa miundombinu ya Umeme  Kinyerezi , Dar es Salaam



Sehemu ya Ujenzi wa Kituo hicho

Mafundi wakiwa kazini

Taswira ya Ujenzi kwa karibu