Zaidi ya Makapuni 56 ya wakala binafsi wa huduma za ajira nchini
yanafanya kazi bila ya kuwa na vigezo vya kisheria kwa mujibu wa sheria ya kazi
ya mwaka 1999.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Habari wa Wizara ya Kazi na Ajira,
Ridhiwani Wema alitanabaisha kuwa, kwa sasa ndio wametangaza maombi ya kusajili
makampuni hayo ambayo yameonekana hayana sifa na vigezo vya kutangaza ajira.
Wema alisema kuwa ni marufuku kwa kampuni yoyote inayojihusisha
na kutangaza ajira kufanya kazi hiyo mpaka pale usajili utakavyokamilika ndio
wataruhusiwa kufanya kazi hiyo
Alivitaja baadhi ya vigezo ambavyo mwombaji anatakiwa kuwanavyo
ni kuwa na katiba ya uwendeshaji wa
kampuni, hati ya usajili wa kampuni, leseni ya biashara, namba ya usajili wa
mlipa kodi, wasifu wa kampuni na kuwa na watu wenye uzoefu na ujuzi.
No comments:
Post a Comment