Na. Mwandishi wetu.
Makampuni matatu makubwa yaliyo ndani ya MeTL Group
hivi majuzi yamefanikiwa kutwaa tuzo za Rais za Watengenezaji Bidhaa kwa mwaka
2013.
Makampuni hayo ni: East Coast Oils & Fats Ltd ya
Kurasini ambayo hutengeneza sabuni na mafuta ya kupikia pamoja na bidhaa
nyingine.
Afritex Limited ambayo hutengeneza Khanga, Vitenge
na bidhaa zifananazo; na 21st Century Textiles ambayo ni kampuni kubwa na ya
kisasa Afrika Mashariki na kati inayotengeneza bidhaa kama khanga, vitenge,
vikoi, mashuka, nguo za kimasai n.k.
Tuzo ya Rais ya Watengenezaji wa Bidhaa ni tuzo
ambayo hutolewa kwa makampuni mbali mbali nchini Tanzania yanayojihusisha na
utengenezwaji wa bidhaa. Ubora wa bidhaa ndio hufanya kampuni kushinda tuzo
hiyo.
No comments:
Post a Comment