CIDA NA PLAN INTERNATIONAL KUPITIA MRADI WA THE MNW PROJECT YATOA MSAADA WA VIFAA VYA TIBA KWA AJILI YA MAMA NA WATOTO MKOANI RUKWA
Dokta Neema Mamboleo mshauri wa Mradi wa Wazazi
na Mwana akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta kitanda maalum kwa
ajili ya kusaidia watoto wachanga waliozaliwa kabla ya muda kutimia na kuwa na
matatizo ikiwa ni sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na mradi huo
Afisa Tawala wa Mradi wa Wazazi na Mwana (MNW)
Bwana Mashauri Ndebile akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta
shehena ya vifaa vya msingi kwa ajili ya kutoa huduma za dharura kwa kina mama
wajawazito na watoto wachanga Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Wilaya ya
Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu
Kimulika Galikunga orodha ya mgao wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya Halmashauri
hiyo
Msaada huo ni sehemu ya misaada mbalimbali ya
mashirikia hayo Mkoani Rukwa ambapo hivi karibuni walitoa msaada wa
"Ambulance" mbili na kujenga vyumba vya upasuaji kwa Halmashauri za
Nkasi na Sumbawanga Vijijini.
No comments:
Post a Comment