Kwa habari zaidi kuhusu ORBIT tembelea tovuti ya: www.orbit-tz.com
KWA MAONI AU USHAURI TUTUMIE KWENYE E-mail: kusinileo@gmail.com

Monday, 9 June 2014

MBUNGE WA MKULANGA ADAM MALIMA ,AMWAGA CHERAHANI KWA WAJASILIAMALI NA VIFAA VYA MICHEZO

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mkulanga Shabani Mandai,(katikati) akiwangalia vijana wa ccm  wakipachika mashine ya cherahani mara baada ya kupokea msaada wa cherahani 20 na kwa ajili ya wajasiliamali na vifaa vyamichezo kutoka kwa Mbunge wa jimbo la Mkulanga ikiwa ni kutekeleza ahadi alizozitoa mbunge wa jimbo hilo kwa wananchi

Mwakilishi wa Mbunge wa Mkulanga ,Omary Kisigalile (kushoto)akimkabidhi mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mkulanga, Shabani Mandai (kulia) Cherehani 20 zilizotolewa na Mbunge wa jimbo hilo kwa ajili ya Vikundi vya wajasiliamali katika kata mbali mbali za wilaya hiyo. Wanaoshuhudia ni Hemed Freji na Catherin Lukas

Katibu wa UVCCM  Wilaya ya Mkulanga Hemed Freji(kushoto) na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mkulanga, Shabani Mandai wakionyesha jezi walizokabidhiwa na mbunge wa Mkulanga ikiwa ni ahadi alizotoa mbunge huyo kwa wananchi katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo na Cherahani kwa ajili ya wajasiliamali

Mwakilishi wa Mbunge wa Mkulanga ,Omary Kisigalile (kulia)akiwakabidhi viongozi wa UVCCM Wilaya ya Mkulanga, sehemu ya  Cherehani 20 zilizotolewa na Mbunge wa jimbo hilo kwa ajili ya Vikundi vya wajasiliamali katika kata mbali mbali za wilaya hiyo.

5-Mwenyekiti wa Vijana na da Catherin wakipachika cherahani mara baada ya kukabidhiwa na mbunge wa Mkulanga kwa ajili ya Vikundi vya wajasiliamali ikiwa ni kutekeleza ahadi za mbunge huyo kwa Wananchi wa jimbo lake

SEHEMU YA CHERAHANI HIZO

Baadhi ya Vijana wa UVCCM Wakishuhudia kukabidhiwa kwa misaada hiyo

Dada Naima Malima akiteta jambo na Mshereheshaji wa siku hiyo.

Mjumbe wa UVCCM Wilaya ya Mkulanga ambaye ni mke wa Mbunge wa Mkulanga Adam Malima, Dada Naima Malima (kulia)akibadilishana Mawazo na Makamanda wa Vijana wa CCM Mkulanga

Viongozi wandamizi wa UVCCM Mkulanga wakifurahia baada ya kuona mzigo wa Cherahani na Vifaa vya michezo ukiingia ukumbini. ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizotoa mbunge wao kwa wananchi. Hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo na Cherahani kwa ajili ya wajasiliamali ilifanyika ,Mkulanga mwishoni mwa wiki.Picha zoote na Kusinigesiblog


No comments:

Post a Comment