Kwa habari zaidi kuhusu ORBIT tembelea tovuti ya: www.orbit-tz.com
KWA MAONI AU USHAURI TUTUMIE KWENYE E-mail: kusinileo@gmail.com

Monday, 28 July 2014

MBUNGE WA TEMEKE ABASS MTEMVU AZIFIKISHA KWA WADAU ZAWADI ZA RAIS KIKWETE

Jul 27, 2014
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu na Mke wake, Mariam wakigawa zawadi za Rais Jakaya Kikwete kwa mdau, walipogawa zawadi hizo kwa viongozi wa CCM na Jumuia za Chama kutoka matawi yote katika jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam, leo, Julai 27, 2014. Zaidi ya wadau 900 walipatiwa zawadi hizo ambazo ni seti za vyombo vya nyumbani, zilitolewa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kwa wabunge wote nchini ili kugawia wadau. Hata hivyo Mtemvu na Mkewe walinogesha kwa kumpatia sadaka ya sh. 10,000 kila mdau waliyemkabidhi zawadi hizo.
 Mke wa Mbunge wa Temeke Mariam Mtemvu, akigawa zawadi hiyo kwa mdau
 Mtemvu na mkewe wakigawa zawadi hizo kwa mdau
 Wadau wakifungasha vizuri zawadi zao baada ya kukavidhiwa na Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu ikiwa ni sehemu ya sadaka ya mwishoni mwa mfungo wa Mwezi Mukufu wa Ramadhani
 Kina mama wa jimbo la Temeke waliopata zawadi hizo wakisubiri kuondoka nazo
Vijana wakiondoka na zwadi zao baada ya kukabidhiwa na Mtembu katika hafla iliyofabyika leo Julai 27, 2014, kwenye Viwanja vya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam. Picha na Bashir Nkoromo-TheNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment