Baadhi ya wafanyabiashara walioudhuria Mkutano wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa
India (IBF),wakichukua chakula
Na Mwandishi Wetu,
Serikali imesema itaendeleza
mapambano dhidi ya rushwa, ubadhilifu wa fedha za umma, urasimu, uzembe katika
ofisi zote za serikali kwa lengo la kukuza na kuimarisha mazingira mazuri na
rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili kukuza uchumi na maendeleo ya
nchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
jana na Jumuiya ya wafanyabiashara wa India (IBF), Waziri wa Sheria na Katiba,
Dk Harrison Mwakyembe alisema kwamba serikali ya awamu ya tano inafanya
marekebisho makubwa ya muundo wake na utendaji kazi ili kukabiliana na
changamoto za muda mrefu katika Nyanja ya biashara na wawekezaji.
Alisema kuwa India ni mwekezaji
mkubwa wa pili nchini Tanzania hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha kwamba
mazingira mazuri na rafiki ya biashara kwa wafanyabiashara wote kutoka Asia
bila kuingiliwa ovyo na watendaji wa serikali.
Waziri huyo wa Sheria na katiba
alikubana na wakati mgumu pale wafanyabiashra hao walivyotoa malalamiko yao kwa
Maafisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Uhamiaji, Wizara ya kazi kuwafuata mara kwa
mara katika mazingira yanachochea rushwa.
“Kweli tumesikia malalamiko ya
wafanyabiashara na usumbufu wa maafisa wa serikali hasa askari wa usalama
barabarani kudai mpaka kadi za manjano na nimewaahidi serikali ya awamu ya tano
itawashughulikia bila kuwaonea aya,” alisema Dk Mwakyembe.
"Naweza kuwahakikishia Rais wa
tano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli yeye ni anatembea kwenye maneno yake
dhidi ya mapambano ya rushwa nchini ambacho ni kikwazo kwa wawekezaji,"
alisema.
Alifafanua kwamba mamlaka za
ukaguzi kuwa nyingi nchini ni swala ambalo serikali inalitizama kwa jicho
makini ili kuleta marekebisho ya kisheria kupunguza usumbufu na kukatisha tamaa
wawekezaji na wafannyabiashara nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo wa Wafanyabiashara India, Bw, Gagan Gupta alisema kuwa Tanzania na
India kiwango cha biashara kimefikia dola za kimarekani milioni 400 na nchi
hizo mbili zimeahidi kuendelea kushirikiana katika mambo ya kiuchumi na
kupunguza vikwazo vya kibiashara.
"Jukwaa hadi sasa linakaribu
wanachama 108 waliosajiliwa na bado wanaendelea kujisajili na sisi jukumu letu
ni kuwaunganisha na mamlaka za serikali zote mbili India na Tanzania,”
aliongeza.
Hivi karibuni, Ubalozi wa India
hapa nchini ulianzisha visa kwa njia ya kieletroniki na kufuta ada kwa
wafanyabiashara wa kitanzania na watanzania wanaotafuta kazi nchini India
katika muendelezo wa kukuza mahusiano wa nchini hizo mbili.
Mwisho.
|
No comments:
Post a Comment