WAZIRI Mkuu Mstaafu
aliyejiuzulu na Mbunge wa sasa wa jimbo la Monduli, Arusha, Edward Ngoyai
Lowassa amesema atahakikisha Tanzania inaondokana na msemo wa kuitwa ‘kichwa
cha mwendawazimu”.
Lowassa
ametamka maneno haya wakati akihutubia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Kaluta jijini Arusha, akitangaza rasmi nia ya kugombea Urais kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Lowassa
‘Mzee wa Maamuzi Magumu’ amese iwapo atapitishwa kugombea kitu cha urais
na kushinda basi atahakikisha anapambana na udhaifu wa Tanzania katika michezo
mbalimbali hadi kufikia kuitwa kichwa cha cha Mwendawazimu.
“Kama
nitapata nafasi, basi nitahakikisha Tanzania inaondokana na kuitwa kichwa cha
Mwendawazimu,” Amesema Lowassa na kuongeza: “Tanzania tumekuwa hatufanyi
vizuri katika michezo mbalimbali ikiwemo riadha na michezo mingine.”
Lowassa
ni kati ya wanachama wa CCM wanaowania nafasi hiyo ya urais kupitia CCM,
wengine wanaotajwa ni Benard Membe, Stephen Wasira, Mwigulu Nchemba na
wengineo.
|
No comments:
Post a Comment